• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FAO yalitaka eneo la Asia na Pasifiki lifanye juhudi kuondoa njaa

  (GMT+08:00) 2018-04-15 19:21:59

  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya chakula na kilimo duniani 'FAO' hivi karibuni limelitaka eneo la Asia na Pasifiki kufanya juhudi kuondoa njaa na kukabiliana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa kilimo.

  Mkutano wa 34 wa eneo la Asia na Pasifiki wa shirika la FAO hivi karibuni ulifanyika huko Fiji, wajumbe kutoka nchi zaidi 40 za eneo la Asia na Pasifiki ambazo ni wajumbe wa FAO walihudhuria mkutano huo.

  Mkurugenzi mkuu wa FAO Bw. Jose Graziano da Silva alisisitiza nchi wanachama wa eneo la Asia na Pacifiki zifanye juhudi kwa kukabiliana na suala la njaa. Alisema kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kwenye eneo hilo imefikia milioni 500, hivyo inahitajika kufanyika kazi nyingi zaidi na kujenga uhusiano thabiti wa urafiki, ili kutimiza lengo la kuondoa njaa lililopo kwenye ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako