• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kujenga nyumba elfu 30 za gharama nafuu kuondoa tatizo la uhaba

  (GMT+08:00) 2018-04-16 08:29:57

  Serikali ya Kenya inapanga kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zipatazo elfu 30 mashariki mwa Nairobi ikiwa sehemu ya ajenda ya maendeleo ya rais Uhuru Kenyatta.

  Akiongea na wanahabari msemaji wa ikulu Manoah Esipisu amesema mradi huo unalenga kujenga nyumba elfu 5 katika eneo la Shauri Moyo, elfu 20 Makongeni, elfu 3 Starehe na elfu mbili eneo la Park Road. Aidha amesema timu inayoongoza ujenzi imepewa miezi sita kuhakikisha ujenzi unaanza.

  Kulingana na takwimu za serikali, Kenya ina uhaba wa nyumba za maana katika miji mingi. Uhaba huo kwa sasa unakadiriwa kufikia majengo laki mbili na nusu kwa mwaka, ingawa makampuni ya nyumba yanaweza kujenga nyumba elfu 50 kwa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako