• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa Russia na Iran wajadili hali ya Syria kwa njia ya simu

  (GMT+08:00) 2018-04-16 08:41:32

  Rais Vladimir Putin wa Russia amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, kujadili hali ya sasa ya Syria baada ya kushambuliwa kwa makombora na Marekani na washirika wake.

  Katika mazungumzo yao pande hizo mbili zimesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani na washirika wake yanakwenda kinyume cha sheria za kimataifa, na yataharibu vibaya mustakbali wa kutatua suala la Syria kisiasa.

  Habari kutoka tovuti ya ikulu ya Russia zimesema Rais Putin amesisitiza kuwa kama vitendo hivyo vikitokea tena, vitaweza kuvuruga hali ya kimataifa.

  Mbali na suala hilo, marais hao wawili pia wamejadiliana kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, na ushirikiano wa kibiashara kati ya Russia na Iran.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako