• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia kujibu jaribio lolote la shinikizo la Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-16 08:49:12

    Mkurugenzi wa idara ya kudhibiti na kutoeneza silaha ya wizara ya mambo ya nje ya Russia Bw. Vladimir Yermakov amesema, Russia itajibu kithabiti jaribio lolote la shinikizo la nguvu kutoka Marekani.

    Akiongea kwenye mkutano wa Baraza la sera za kidiplomasia na ulinzi Bw. Yermakov amesema, wanaona katika miaka kumi na tano iliyopita, mazingira ya teknolojia ya kijeshi yamebadilika na kuwa mazuri zaidi kwa Russia. Hivyo kwa hali yoyote wanaweza kujibu vikali majaribio yoyote ya shinikizo la nguvu kutoka Marekani.

    Ameongeza kuwa mashindano ya silaha siku hizi yamekuwa hatari zaidi kutokana na hatua za baadhi ya nchi za magharibi vikiwemo vikwazo, ulazimishaji na vitendo kati ya mataifa visivyo na maadili vinavyofanywa na nchi hizo kutokana na kutotaka kutambua utaratibu mpya wenye ncha nyingi.

    Amesisitiza kuwa kwa mujibu wa mtazamo huo, mashindano ya silaha sio mzaha tu, kwa kuwa yana madhara makubwa ya kudumu kwa utulivu wa dunia na usalama wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako