• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu ufumbuzi wa kisiasa nchini Libya

  (GMT+08:00) 2018-04-16 08:53:05

  Balozi mdogo wa China nchini Libya Bw. Wang Qimin amesema, China inaunga mkono ufumbuzi wa kisiasa uliotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Libya.

  Mwanadiplomasia huyo wa China amesema hayo baada ya kuwa na mazungumzo na mkuu mpya wa baraza la juu la Libya Bw. Khaled al-Meshri mjini Tripoli.

  Bw. Wang amesisitiza umuhimu wa Libya kufanya uchaguzi wa bunge na wa rais ili walibya waweze kujiamulia mustakabali wao, akiongeza kuwa mambo hayo yatatimizwa kwa njia ya kuunga mkono mwongozo wa Umoja wa Mataifa.

  Pia amesisitiza umuhimu wa kufanya mkutano wa kitaifa uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa katika miji kadhaa nchini Libya, kwani utawawezesha watu wa Libya kujadili matatizo yao na njia bora za kukomesha migogoro.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako