• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Amani na utulivu nchini Sudan ni vipaumbele kwenye mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Sudan

  (GMT+08:00) 2018-04-16 09:08:57

  Mkurugenzi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Sudan Bw. Jean-Michel Dumond amesema, amani na utulivu nchini Sudan ni vipaumbele vya mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Sudan.

  Bw. Dumond ameyasema hayo jana wakati alipofanya mazungumzo na Msaidizi wa Rais wa Sudan Bw. Faisal Hassan Ibrahim huko Khartoum.

  Akiongea na wanahabari baada ya mazungumzo hayo Bw. Dumond alisema wamezungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya pande hizo mbli, mchakato wa amani na maendeleo ya kisiasa nchini Sudan.

  Aidha alimwelezea msaidizi wa rais wa Sudan juhudi za Umoja wa Ulaya za kuunga mkono maendeleo ya Sudan, hasa katika suala la Darfur, suala la wakimbizi na usalama wa chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako