• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yajitahidi kutimiza ongezeko la asilimia 8 ifikapo mwaka 2022

    (GMT+08:00) 2018-04-16 09:09:01

    Waziri wa mipango wa Misri Bi. Hala al-Said amesema mpango wa maendeleo endelevu wa Misri unalenga kufikia ongezeko la asilimia 8 ifikapo mwaka 2022. Bi. Al-Said amesema kutimiza lengo hilo kunahitaji kuongeza viwango vya akiba na uwekezaji kutoka asilimia 7.3 na asilimia 16.9 ya sasa hadi kufikia asilimia 20 na asilimia 25.6 mtawalia ifikapo mwaka 2021/2022. Misri imeshuhudia kudidimia kwa uchumi katika miaka kadha iliyopita kutokana na machafuko ya kisiasa na kiusalama, na ilizindua mpango wa mageuzi ya kiuchumi tangu 2016, ikihamasishwa na mkopo wa dola bilioni 12 kutoka kwa IMF, ambao nusu ya fedha hizo tayari zimeshatolewa kwa Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako