• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaongoza kwa kushinda medali kwa nchi za Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-04-16 10:30:42

    Mashindano ya jumuiya ya madola yamemailizika jana kwa wenyeji Australia kushika nafasi ya kwanza kwa kutwaa medali nyingi, ambapo walishinda medali 198, dhahabu 80, fedha 59 na shaba 59, ikiwa ni kati ya jumla ya medali 840 zilizoshindaniwa, 275 dhahabu, 276 fedha na 289 shaba.

    Bara la Afrika kwa ujumla wake lilishinda medali 96 kati ya hizo 840, na timu ya Afrika Kusini ikiwa ndiyo kinara kwa Afrika kwa kushinda medali 37, 13 za dhahabu, 11 za fedha na 13 za shaba.

    Timu ya Kenya ndiyo imekuwa kinara kwa mataifa ya Afrika Mashariki kwa kutwaa medali nyingi ambapo imeshinda 17, 4 za dhahabu, 7 fedha na 6 shaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako