• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simon Msuva wa Tanzania: aendelea kung'ara ligi kuu ya Morocco, afunga magoli mawili yaliyoiokoa timu yake

  (GMT+08:00) 2018-04-16 10:31:13

  Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva jana ameifungia mabao mawili timu yake, Difaa Hassan El Jadida yaliyoifanya ipate sare ya 3-3 ikiwa ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya wenyeji, Olympique de Khouribga Uwanja wa Phosphate mjini Khouribga.

  Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Jadida na ikifikisha pointi zake 38 baada ya kucheza mechi 25.

  Msuva amefunga mabao yake dakika za 65 na dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, hilo likiwa bao lililoinusuru Jadidi kupoteza mechi leo na kuibuka shujaa wa timu yake, wakati bao lingine la timu hiyo limefungwa na Tarik Astati dakika ya 33.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako