• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Man City ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza msimu huu

  (GMT+08:00) 2018-04-16 10:54:57

  Manchester City ndiyo mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kufikisha pointi 87 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki mashindano hayo msimu huu.

  Ubingwa wa City umewezekana baada ya timu inayoshika nafasi ya pili Manchester United kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Westbrom Albion jana.

  United ambayo sasa inasaliwa na pointi zake 71 ikiwa bado na michezo 5, ambapo hata ikishinda yote haiwezi kufikisha pointi 87.

  Huu ni ubingwa wa tano kwa City katika soka la daraja la juu la Uingereza ikiwa ni ubingwa wa tatu tangu kuanzishwa kwa zama mpya ya ligi, na kwa kocha Pep Guardiola huu ni ubingwa wake wa kwanza wa ligi akiwa na timu hiyo.

  Na katika mechi nyingine iliyopigwa jana Newcastle imeinyuka Arsenal 2-1 na rekodi mbaya ikiendelea kumuandama Arsene Wenger.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako