• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makampuni ya serikali kuu ya China yaendelea vizuri katika robo ya kwanza mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-04-16 16:43:24

  Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa mali za taifa ya baraza la serikali ya China imesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, mapato ya makampuni yanayomilikiwa na serikali kuu yalifikia yuan trilioni 6.4, sawa na dola za kimarekani zaidi ya trilioni moja, ambalo ni ongezeko la asilimia 8.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, msemaji wa kamati ya usimamizi na uendeshaji wa mali za taifa ya baraza la serikali ya China Bw. Peng Huagang amesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, mapato ya makampuni yanayomilikiwa na serikali kuu yameongezeka kwa utulivu, haswa mapato ya makampuni ya sekta za umeme, makaa ya mawe, mashine na biashara yameongezeka kwa kasi zaidi. Bw. Peng anasema,

  "Katika robo ya kwanza, makampuni ya serikali kuu yamepata faida zaidi ya renminbi yuan bilioni 377, sawa na dola za kimarekani karibu bilioni 60, ambalo ni ongezeko la asilimia 20.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Mwezi Machi pekee, faida hiyo ilikuwa yuan karibu bilioni 170, na kuvunja rekodi katika historia."

  Katika robo ya kwanza, makampuni yanayomilikiwa na serikali kuu yameendelea na juhudi za kupunguza gharama na madeni, na kufanikiwa kupunguza kwa asilimia 0.5 na 0.4.

  Aidha ushuru uliotolewa na makampuni hayo umeendelea kuongezeka, Bw. Peng anasema,

  "Katika robo ya kwanza, makampuni ya serikali kuu yametoa ushuru zaidi ya yuan bilioni 587, ambalo ni ongezeko la asilimia 10.6 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Kati ya makampuni hayo, ushuru uliotolewa na makampuni ya makaa ya mawe na mawasiliano ya barabarani umeongezeka kwa asilimia 20, na ule uliotolewa na makampuni ya mafuta, madini, umeme na biashara umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 15."

  Bw. Peng anaona kuwa katika miaka miwili iliyopita, sababu ya kukua vizuri kwa makampuni yanayomilikiwa na serikali kuu ni maendeleo ya utulivu ya uchumi, mageuzi ya utoaji, na mageuzi ya makampuni hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako