• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya 4 ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan yafanyika

    (GMT+08:00) 2018-04-16 17:46:21

    Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Japan Bw. Kouno Tarou leo huko Tokyo wameendesha mazungumzo ya nne ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya China na Japan.

    Katika mazungumzo hayo, Bw. Kouno Tarou amesema, ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Japan ni msingi muhimu na nguvu ya kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Amesema kwa kukabiliana na mabadiliko mapya ya hali ya nchi hizo mbili na ya dunia, Japan inapenda kushirikiana na China kukuza ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo.

    Kwa upande wake, Bw. Wang Yi amesema, kwa sasa ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Japan umekabiliana na hali mpya ya kihistoria na mazingira ya jumla, na uko katika mwanzo mpya. Pande hizo mbili zinapaswa kuwasiliana zaidi, ili kuongeza maelewano na uaminifu, kuhimiza uratibu na kusukuma mbele zaidi ushirikiano.

    Mazungumzo ya ngazi ya juu ya uchumi kati ya nchi hizo yamefanyika tena baada ya miaka minane kupita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako