• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama lalaani shambulizi dhidi ya kikosi cha ulinzi wa amani nchini Mali

  (GMT+08:00) 2018-04-16 17:52:22

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likilaani vikali shambulizi lililofanywa na watu wenye silaha dhidi ya kikosi cha kulinda amani cha umoja huo huko Timbuktu nchini Mali.

  Shambulizi hilo lililotokea jumamosi iliyopita mjini Timbuktu na kusababisha kifo cha askari mmoja wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kutoka Burkina Faso na watu wengine zaidi 10 kujeruhiwa.

  Taarifa hiyo imesema, nchi wanachama wa Baraza la Usalama zimeisisitiza serikali ya Mali ifanye uchunguzi kuhusu shambulizi hilo kwa haraka na kuwafikisha watuhumiwa mbele ya sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako