• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makamishna watatu wajiuzulu kutoka Tume ya uchaguzi Kenya

  (GMT+08:00) 2018-04-16 19:38:02

  Makamishna watatu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) wamejiuzulu, wakisema wamechukua uamuzi huo kwa kutokuwa na imani na mwenyekiti wao.

  Makamu mwenyekiti Consolata Nkatha, na makamishna Paul Kurgat na Margaret Mwachanya wamewaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kuwa kwa muda mrefu na mara nyingi sana, mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati ameshindwa kuwa na msimamo na kuongoza tume hiyo wakati wa matatizo na kutoa maelekezo pale inapotakiwa.

  Wataalam wanasema, hatua hiyo itayumisha tume hiyo katika wakati ambao inajiandaa kufanya tathmini ya mipaka ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako