• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria yataka uchunguzi wa wazi usio na upendeleo na wa uhakika kuhusu matumizi ya silaha za kemikali

    (GMT+08:00) 2018-04-16 20:06:12

    Naibu waziri wa ulinzi wa Syria Faisal Mekdad amesema serikali yake iko tayari kushirikiana na wachunguzi kutoka Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) walioko nchini humo.

    Bw. Mekdad amesema wachunguzi hao waliwasili mjini Damascus siku tatu zilizopita na wamekutana na upande wa serikali ya Syria, ambapo pande zote mbili zilijadili ushirikiano kwa ajili ya timu hiyo kufanya kazi zake kwa uwazi, bila upendeleo, na kwa uhakika. Pia amesisitiza utayari wa serikali ya Syria katika kushirikiana na kuwezesha kazi za timu hiyo inayochunguza tuhuma dhidi ya jeshi la serikali kutumia silaha za kemikali katika eneo la Douma lililokuwa linashikiliwa na waasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako