• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuunda mfumo wa biashara ya pande nyingi

  (GMT+08:00) 2018-04-16 20:13:11

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, sera za Marekani za kujilinda kibiashara na kitendo cha upande mmoja ambacho si kama zitaharibu maslahi ya China tu bali pia kuharibu mfumo wa biashara ya pande nyingi na maslahi ya nchi mbalimbali.

  Amesema hivi karibuni, Australia iliendelea kujitahidi kufungua uchumi na biashara huria, na kwamba nchi hiyo inafuatilia hatua za Marekani za kuongeza ushuru kwa baadhi ya wenzi wa kibiashara.

  Bibi Hua amesema, msimamo huo wa Australia umewakilisha maoni ya jumuiya ya kimataifa. Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kupinga kitendo cha upande mmoja na mfumo wa kujilinda kibiashara ili kudumisha mfumo wa biashara ya pande mbalimbali na kujenga uchumi wazi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako