• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Afrika Kusini atangaza mpango wa kuvutia uwekezaji

  (GMT+08:00) 2018-04-17 09:01:21

  Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa mkutano wa uwezekaji baadaye mwaka huu na kutarajiwa kuvutia randi trilioni 1.2 sawa na dola bilioni 100 za Kimarekani katika miaka mitano ijayo.

  Akitoa tangazo hilo jana kabla ya kuondoka kwenda London kuhudhuria mkutano wa wakuu wa serikali wa Jumuiya ya Madola, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema ataendelea kutoa mwaliko kwa wawekezaji wanaoongoza na viongozi wa biashara kuhudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika Agosti au Septemba mwaka huu. Aidha amesema mkutano huo utakaoshirikisha wawekezaji wa ndani na nje, hautazungumzia mazingira ya uwekezaji pekee bali pia unatarajiwa kuripoti makubaliano ya uwekezaji halisi ambayo yameshafikiwa na kutoa jukwaa kwa wawekezaji kutafuta fursa katika soko la Afrika Kusini.

  Amewahakikishia watu kuwa mkutano huo utakuwa na matokeo halisi yanayoweza kutimizwa kwa haraka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako