• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Geneva yasherehekea Siku ya Lugha ya Kichina

  (GMT+08:00) 2018-04-17 09:01:39

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Michael Moller amesema Umoja wa Mataifa unafurahia kuihesabu China kama mwenza muhimu.

  Akiongea wakati wa ufunguzi wa maonesho ya "Mvuto wa Utamaduni wa China: Kutoka Maandiko hadi Fasihi", katika sherehe ya Siku ya Lugha ya Kichina, ambayo ni moja ya siku zilizopangwa na UN kwa lugha zake zote kuu sita, Bw. Moller amesema China ikiwa moja ya wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, inabeba jukumu muhimu katika ujenzi wa amani na usalama duniani.

  Pia ameelezea mafanikio ya China katika kuwatoa mamilioni ya watu kwenye umasikini mkali na utendaji wake katika malengo mengi ya Maendeleo ya Milenia.

  Kwa upande wake mjumbe wa kudumu na balozi wa China katika Ofisi ya Umoja Mataifa ya Geneva, Yu Jianhua, amesema moja ya maandiko ya Kichina yanayotumika hivi leo na kubeba umuhimu wa kuelewa falsafa ya China ni "Min" likiwa na maana ya "Umma". Amesisitiza kuwa ni wazo kuu la kuweka watu kwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako