• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia na UM zakubaliana kusukuma mbele ushirikiano wa kulinda amani

  (GMT+08:00) 2018-04-17 09:12:23

  Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia imetoa taarifa ikisema, nchi hiyo na Umoja wa Mataifa wamekubaliana kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa kulinda amani.

  Taarifa hiyo imesema, makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya naibu katibu mkuu wa Umoja huo Bw. Jean-Pierre Lacroix na naibu waziri wa wizara hiyo Bw. Hirut Zemene.

  Bw. Lacroix amepongeza mchango uliotolewa na Ethiopia kwa miaka 60 katika ulinzi wa amani ulioanzia vita vya Korea mwaka 1950 hadi 1953 hadi leo katika operesheni ya kulinda amani haswa katika nchi za kanda ya pembe ya Afrika zinazokumbwa na matatizo kama Somalia.

  Kwa upande wake, Bw. Zemene ametoa wito kwa Umoja huo na nchi washirika wake kutoa msaada wa kutosha kwenye operesheni za kulinda amani ambazo askari wa nchi hiyo wanashiriki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako