• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa watangaza kurejea kwa wakimbizi 53 wa Sudan kutoka Chad

    (GMT+08:00) 2018-04-17 09:12:47

    Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetangaza kuwa wakimbizi 53 wa Sudan wamerudi nyumbani baada ya kukaa kwa miaka 14 kwenye kambi ya wakimbizi iliyoko mashariki mwa Chad.

    Kwenye taarifa Shirika hilo pamoja na kamishna wa wakimbizi wamepongeza msafara wa wakimbizi 53 wa Sudan ambao wamerudi makwao baada ya kukaa kwa miaka zaidi ya 14 nchini Chad.

    Mwakilishi wa shirika hilo nchini Sudan Bi Noriko Yoshida amesema, inafurahisha kuona wakimbizi hao wamerudi nyumbani kwao baada ya kuishi ukimbizini kwa miaka mingi. Pia ameitaka jumuiya ya kimataifa kusaidia juhudi za serikali ya Sudan katika kurejesha wakimbizi wake kutoka Chad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako