• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pendekezo la Ukanda mmoja Njia moja latajwa kuwa linatoa fursa za maendeleo nchi za kiarabu

  (GMT+08:00) 2018-04-17 09:14:27

  Mchumi mashuhuri wa Umoja wa Falme za kiarabu UAE Bw. Nasser Saidi amesema pendekezo la Ukanda mmoja Njia moja la China ni fursa kwa nchi za Kiarabu kuziba pengo la uwekezaji kwenye miundombinu na kuinua sekta zake za uchumi hadi kufikia ngazi mpya. Akihutubia Mazungumzo ya Njia mpya ya hariri, yaliyoandaliwa na Chuo cha Kennedy cha Chuo kikuu cha Harvard, Bw. Saidi amesema wakati muundo wa uchumi wa dunia unaelekea Mashariki, nchi za kiarabu zinapaswa kutumia vizuri fursa zinazotolewa na Ukanda mmoja Njia moja, na kushirikiana zaidi na China kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo nishati safi, sayansi ya viumbe na ujenzi wa Kituo cha anga za juu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako