• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika alaani matishio ya mabomu nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-04-17 09:30:14

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Francisco Madeira jana alizitaka pande mbalimbali zifanye juhudi ili kuondoa matishio ya mabomu yaliyotengenezwa kienyeji IED dhidi ya vikosi vya usalama na raia nchini Somalia.

    Bw. Madeira amesema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa kupambana na mabomu ya kienyeji. Amesema matumizi ya mabomu hayo yamekuwa tishio kuu kwa utulivu wa nchi hiyo, na ametaka suala hilo litatuliwe kihalisi.

    Bw. Madeira amesisitiza kuwa, njia bora ya kutokomeza mabomu hayo ni kuwa na siasa sahihi. Vilevile ametaka jeshi, askari polisi na serikali washirikiane kupambana na matumizi ya mabomu ya kienyeji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako