• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yafikiria kuiwekea Russia vikwazo vingi zaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-17 09:47:00

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Sarah Sanders amesema, Marekani inafikiria kuiwekea Russia vikwazo vingine na uamuzi husika utatolewa hivi karibuni.

    Bibi Sanders amesema, rais Donald Trump wa Marekani atachukua msimamo wenye nguvu dhidi ya Russia, lakini pia anapenda kukutana na rais Vladimir Putin wa Russia.

    Amesema sera ya Marekani ya kuendelea na mapambano dhidi ya kundi lenye siasa kali la Islamic State nchini Syria haitabadilika. Ingawa rais Trump anataka kurejesha jeshi la Marekani kutoka Syria, lakini hakuna ajenda halisi ya kuondoa jeshi hilo. Amesema Marekani inatumai kuwa nchi nyingine zikiwemo za sehemu ya Ghuba zitajihusisha katika hatua hiyo na kutoa msaada wa fedha kwa operesheni za kijeshi nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako