• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweka hatua za kupinga kwa muda uagizaji wa mtama kutoka Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-17 16:24:44

    Wizara ya biashara ya China leo imetangaza uamuzi wa kuzuia kwa muda mtama unaoagizwa kutoka Marekani kwa bei nafuu baada ya uchunguzi uliogundua kuwa maagizo hayo yameathiri soko la ndani la nafaka hiyo.

    Wizara hiyo imesema, uuzaji wa mtama kutoka Marekani kwa bei nafuu umeharibu sekta ya uzalishaji wa mtama na pia umesababisha hasara nchini China, hivyo imeamua kuweka hatua za kupinga kwa muda uingizaji wa mtama unaoagizwa kutoka Marekani.

    Kwa mujibu wa uamuzi huo, kuanzia kesho tarehe 18, wafanyabiashara wanapoagiza mtama kutoka Marekani wanapaswa kutoa dhamana ya asilimia 178.6 kwa forodha ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako