• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yatoa jukwaa muhimu kwa biashara kati ya China na Afrika

  (GMT+08:00) 2018-04-17 17:33:38

  Maonesho ya 123 ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yamefunguliwa tarehe 15. Katika miaka mingi iliyopita, maonesho hayo yametoa jukwaa muhimu kwa ajili ya kuhimiza biashara kati ya China na nchi nyingine duniani, zikiwemo nchi za Afrika.

  Katika miaka ya hivi karibuni, Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yamejitahidi kutekeleza pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja, ili kuongeza ushirikiano wa biashara na uwekezaji kati ya China na dunia nzima. Msemaji wa maonesho hayo ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya Biashara za kimataifa ya China Bw. Xu Bing amesema, kutokana na kusukumwa mbele kwa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", nchi zinazohusika zikiwemo zile za Afrika zimekuwa sehemu muhimu ya maonesho hayo. Anasema,

  "Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou ni jukwaa muhimu la kuhimiza biashara kati ya China na nchi za Afrika. Naamini kuwa kutokana na maendeleo ya uchumi wa Afrika na ubora wa bidhaa za China, wafanyabiashara wengi zaidi wa Afrika watakuja kushiriki kwenye maonesho hayo."

  Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki alipohojiwa na waandishi wetu wa habari amesema, Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yamerahisisha ushirikiano kati ya wafanyabiashara na wazalishaji bidhaa.

  Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yalianzishwa mwaka 1957, ni maonesho makubwa na yenye historia ndefu zaidi ya kimataifa ya bidhaa nchini China. Bw. Anieke Benjamin Cheibuzor ni mfanyabiashara kutoka Nigeria. Anasema, "Kwanza nataka kununua vifaa vya uchunguzi wa usalama. kwa bahati nzuri nimepata vifaa hivyo vizuri vyenye bei nafuu. Aidha, nataka kununua bidhaa nyingine zinazotumiwa sana na wateja wa Nigeria zikiwemo mitambo ya kutumia nishati ya jua, na simu za ndani."

  Bw. Xu Bing ameeleza kuwa ili kutekeleza mkakati wa kitaifa, China ilitoa mpango wa kuboresha zaidi Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou mwaka 2015. Hadi sasa maonesho hayo yamekamilisha mifumo mipya kadhaa ikiwemo mfumo wa kutafuta bidhaa na wa ramani kwenye mtandao wa Internet na simu ya mkono.

  Maonesho ya 123 ya kimataifa ya Biashara ya Guangzhou yataendelea mpaka tarehe 5 Mei, na yanashirikisha mashirika zaidi ya elfu 25 kutoka China na nchi za nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako