• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yaitaka OPCW kuharakisha kuchunguza shutuma dhidi ya Syria kutumia silaha za kemikali

    (GMT+08:00) 2018-04-17 18:34:54

    Mjumbe wa Russia katika Baraza la Shirika la Kupinga Matumizi ya Silaha za Kemikali OPCW, Bw. Alexander Shulkin amelitaka shirika hilo kuchunguza haraka shutuma dhidi ya shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria.

    Bw. Shulkin amesema, Marekani, Uingereza na Ufaransa zimefanya shambulizi la kijeshi dhidi ya Syria kabla ya shirika hilo kutoa ripoti yake juu ya shutuma hiyo, kitendo kilichoonyesha kwamba, nchi hizo zimehukumu Syria ina makosa kabla ya uchunguzi kumalizika.

    Amesisitiza kuwa shambulizi hilo lililofanywa bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekiuka katiba ya Umoja huo na linaweza kuchukuliwa kama uvamizi.

    Habari zinasema, madaktari wa kijeshi na wataalam wa kuzuia silaha za kemikali wa Russia hawajapata uthibitisho wowote wa Syria kutumia silaha za kemikali zilizosababisha vifo kwa raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako