• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pemba-Mafuta ya makonyo yapata soko la uhakika China

  (GMT+08:00) 2018-04-17 19:12:53

  Kiwanda cha mafuta ya makonyo kilichopo Wawi Pemba ambacho ndicho pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuzalisha mafuta hayo,kimepata soko la uhakika China.

  Kiwanda hicho kimetiliana saini makubaliano na kampuni ya Kunshan Asia Aroma ya China kuongeza uzalishaji wa mafuta hayo ambayo mahitaji yake yameongezeka katika soko la China.

  Mkurugenzi mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC),Dk Said Mzee alisema makubaliano hayo yatakiwezesha kiwanda kuwa na uwezo wa kuzalisha mafuta hadi tani 2,000.

  Alisema ukarabati wa kiwanda hicho utahusisha njia ya pili ambayo itatoa nafasi ya uzalishaji wa mafuta yanayotokana na bidhaa za chakula.

  Katika hatua hiyo ya ukarabati,kampuni ya Kunshan Aroma itawekeza jumla ya Sh.2 bilioni ,ikiwemo uwekeaji wa mitambo mipya ya uzalishaji wa bidhaa za vyakula.

  Dk.Mzee alisema hayo kwa kiasio kikubwa yataongeza juhudi za uzalishaji wa karafuu na kukidhi mahitaji ya mafuta yanayozalishwa kiwandani hapo.

  Aidha alisema juhudi zinakwenda sambamba na mikakati ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuongeza uzalishaji wa zao la karafuu pamoja na bidhaa zake kwa ujumla yakiwamo mafuta ya makonyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako