• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • satelaiti ndogo ya kisasa ya Afrika iko tayari kurushwa

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:33:56

    Satelaiti kubwa zaidi na ya kisasa zaidi yenye umbo la mchemraba katika Afrika iko tayari kurushwa.

    Waziri wa sayansi na teknolojia wa Afrika Kusini Bw. Mmamoloko Kubayi-Ngubane ametangaza habari hiyo katika Chuo Kikuu cha CPUT mjini Cape Town wakati alipohudhuria hafla ya kupeleka satelaiti hiyo nchini India ambako itarushwa mwezi Julai.

    Satelaiti hiyo iitwayo ZACUBE-2 yenye uzito wa kilo 4 imeendelezwa na chuo hicho cha CPUT kwa kushirikiana na Taasisi ya teknolojia kati ya Ufaransa na Afrika Kusini.

    Satelaiti hiyo itafuatilia meli zilizoko kwenye pwani ya Afrika Kusini na kugundua haraka moto unaotokea misituni kupitia kamera maalumu iliyobuniwa na Baraza la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Afrika Kusini CSIR.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako