• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa Afrika waapa kuendelea na vita dhidi ya ufisadi na uhamishaji haramu wa fedha

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:39:47

    Mawaziri wa Afrika wamesisitiza azma yao ya kupambana na ufisadi na uhamishaji haramu wa fedha nje ya bara la Afrika ambao unaigharimu bara hilo zaidi ya dola bilioni 50 za Kimarekani.

    Kauli hiyo wameitoa kwenye mkutano wa pili wa mwaka wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia. Akiongea kwenye mkutano wa mawaziri, kamishna wa Umoja wa Afrika wa mambo ya kijamii Amira El Fadil amesema ufisadi ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya Afrika, na kusisitiza kuwa utawala bora kupitia mapambano dhidi ya ufisadi ndio msingi wa mageuzi ya bara hilo. Kwa mujibu wa Bi. Fadil, Umoja wa Afrika umekuwa ukishirikiana na taasisi nyingine za jumuiya hiyo kugundua uhamishaji haramu wa fedha unaotokana na ufisadi.

    Mkutano huo wa siku sita unaohusisha kamati ya kiufundi ya fedha, mambo ya fedha, mipango ya kiuchumi na mafungamano umemalizika jana huko Addis Ababa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako