• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yavunja njama ya mashambulizi ya kigaidi

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:40:32

    Idara ya usalama ya Russia FSB imesema wanausalama wametibua njama ya kufanya mashambulizi ya kigaidi kwenye jimbo la Rostovskaya, lililoko kusini magharibi mwa Russia. Taarifa iliyotolewa na idara hiyo kwenye tovuti yake inasema wanausalama waligundua na kutokomeza genge moja lenye siasa kali linalounga mkono kundi la Islamic State, ambalo limeagizwa na kundi la IS kupanga mashambulizi kwa kutumia mabomu na bunduki jimboni humo. Taarifa inasema kwenye operesheni hiyo watu watatu wa genge hilo wamekamatwa wakiwa na silaha na mabomu ya kienyeji, na kiongozi wa genge hilo alijipua wakati wa kukabiliana na wanausalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako