• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itajibu kwa hatua madhubuti kama Marekani ikiendelea kufanya umwamba na kutojali

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:40:36

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema endapo Marekani itaendelea kufanya umwamba na kutojali bila kujizuia na kwenda kinyume na mkondo wa maendeleo, hakika China itajizatiti na kuijibu kwa hatua madhubuti, na kushinda vita hii ya kulinda utaratibu wa pande nyingi na uhuru wa biashara.

    Bibi Hua Chunying ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia mgogoro wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani. Amesema China ikiwa nchi kubwa yenye kuwajibika, inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, kutafuta ushirikiano kwa kufungua mlango na kwa njia ya kunufaisha pande zote, ili kuchangia zaidi katika kuleta utulivu na mustakabali mzuri kwa dunia nzima.

    Amesema hivi karibuni jumuiya ya kimataifa imeitaka Marekani iheshimu Shirika la biashara duniani WTO na kanuni za utaratibu wa pande nyingi. Watu wengi nchini Marekani pia wanapinga vitendo hivyo vya Marekani vinavyojiharibia na pia kuharibu nchi nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako