• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Russia na Ujerumani wazungumzia hali ya Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-18 09:41:01

    Rais Vladimir Putin wa Russia amezungumza kwa njia ya simu na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel. Pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea na juhudi za kidiplomasia kwa ajili ya utatuzi wa suala la Syria, ikiwa ni pamoja na kupitia mazungumzo ya amani ya Geneva na Astana.

    Habari kutoka Tovuti ya Ikulu ya Kremlin zimesema, viongozi wa nchi hizo mbili wamebadilishana maoni kuhusu Marekani na washirika wake kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria, na wameahidi kudumisha mawasiliano kuhusu suala hilo katika siku za baadaye.

    Rais Putin amesisitiza kuwa, vitendo vya kimabavu vya Marekani na washirika wake vimeharibu kanuni za kisheria ikiwemo katiba ya Umoja wa Mataifa, hatua ambayo imehujumu vibaya mchakato wa kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako