• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brighton & Hove Albion yaanza kampeni ya kujinusuru isishuke daraja la ligi kuu

    (GMT+08:00) 2018-04-18 10:39:11

    Timu ya Brighton & Hove jana imefanikiwa kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutoshuka daraja kwenye ligi kuu nchini Uingereza baada ya kutoka sare ya magoli 1-1 ilipocheza dhidi ya Tottenham Hotspurs jana usiku.

    Sare hiyo inaifanya Brighton ambayo ipo katika nafasi ya 13 ifikishe pointi 36 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

    Brighton walipata goli lao kwa njia ya penati kupitia Pascal Gross kwa njia ya penati likiwa ni la kusawazisha baada ya Harry Kane kufunga goli la kuongoza la Tottenham.

    Katika mechi hii, Kocha wa Tottenham aliwapumzisha baadhi ya wachezaji ikiwa ni kwa ajili ya mechi ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester united jumamosi ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako