• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafanya mipango ya ngazi tofauti ili kukabiliana na mvutano wa kibiashara na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-18 16:15:02

    Msemaji wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Yan Pengcheng leo amesema, China imefanya mipango ya ngazi tofauti na akiba ya sera kwa ajili ya kukabiliana na mvutano wa kibiashara uliochochewa na Marekani.

    Kwa mujibu wa tathmini ya jumla, athari ya mvutano huo kwa uchumi wa China ni ndogo, pia inadhibitika, na China ina imani, mazingira na uwezo wa kudumisha uchumi wake uendelezwe kwa utulivu.

    Bw. Yan Pengcheng amesema, kwa upande mmoja, hatua ya kujilinda kibiashara ya Marekani inaleta athari kwa uuzaji bidhaa wa makampuni ya baadhi ya sekta ya China, na kuongeza shinikizo kwa ajira, kwa upande mwingine, wateja wa Marekani na makampuni ya uzalishaji wa sekta husika pia yatapata hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako