• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kutoa orodha mpya ya sekta za kupiga marufuku uwekezaji kutoka nchi za nje

  (GMT+08:00) 2018-04-18 16:56:26

  Kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China leo imesema, China itatoa orodha mpya ya sekta za kupiga marufuku uwekezaji kutoka nchi za nje, na kupunguza sekta hizo kwa kiasi kikubwa, ili kufungua mlango zaidi kwa sekta muhimu za kiuchumi.

  Msemaji wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Yan Pengcheng kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo amesema, orodha mpya ya sekta za kupiga marufuku uwekezaji kutoka nchi za nje ni waraka muhimu wa kupunguza vizuizi dhidi ya uwekezaji kutoka nchi za nje, na itatekelezwa mapema kadiri iwezekanavyo kabla ya mwezi Julai mwaka huu. Bw. Yan anasema,

  "Tutapunguza zaidi vizuizi dhidi ya uwekezaji kutoka nchi za nje kwa kiasi kikubwa. Si kama tu tutapunguza sekta za uchumi za kupiga marufuku uwekezaji kutoka nchi za nje, bali pi tutakuwa na nia kubwa zaidi ya kuhimiza ufunguaji mlango katika sekta muhimu."

  Katika orodha hiyo mpya, sekta za utengenezaji zitazingatiwa zaidi. Kwa mfano, sekta ya utengenezaji wa magari itatekeleza utaratibu wa kufungua mlango kwa kipindi cha mpito, na mwaka huu China itaondoa masharti ya asilimia ya hisa ya wawekezaji wa nchi za nje katika makampuni ya magari maalumu na yale yanayotumia nishati mpya, mwaka 2020, masharti hayo yataondolewa katika makampuni ya magari ya kibiashara, na mwaka 2022 masharti hayo yataondolewa katika makampuni ya magari ya aina yote.

  Mbali na magari, katika sekta za kutengeneza meli na ndege, masharti hayo pia yataondolewa kabisa mwaka huu. Bw. Yan anasema,

  "Licha ya sekta za fedha na magari, China pia itachukua hatua zaidi ya kufungua mlango katika sekta za nishati, maliasili, miundombinu, mawasiliano ya barabara, usafirishaji wa bidhaa na huduma maalumu."

  Bw. Yan ameeleza kuwa, hatua ya kufungua mlango zaidi katika sekta za utengenezaji imeonesha msimamo wa China wa kupinga vitendo vya kujilinda kibiashara, na kuunga mkono kithabiti utandawazi. Bw. Yan pia amesema China inahimiza makampuni ya China na nchi za nje kufanya ushirikiano wa mitaji, teknolojia, uendeshaji na watu katika nyanja zaidi, na China itachukua hatua zaidi ili kuanzisha mazingira yenye usawa na kurahisisha shughuli za uwekezaji. Anasema,

  "China itayatendea mashirika ya ndani na nchi za nje kwa usawa katika maagizo ya serikali, utungaji wa vigezo, miradi ya teknolojia na utaratibu wa kuandikisha. Pia itaongeza nguvu za kulinda haki miliki, na kuhakikisha maslahi halali ya wawekezaji kutoka nchi za nje."

  Kuhusu mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani, Bw. Yan amesema, China imefanya mipango ya ngazi tofauti na akiba ya sera kwa ajili ya kukabiliana na mvutano huo uliochochewa na Marekani.

  Kwa mujibu wa tathmini ya jumla, athari ya mvutano huo kwa uchumi wa China ni ndogo, pia inadhibitika, na China ina imani, mazingira na uwezo wa kudumisha uchumi wake uendelezwe kwa utulivu.

  Bw. Yan Pengcheng amesema, kwa upande mmoja, hatua ya kujilinda kibiashara ya Marekani inaleta athari kwa uuzaji bidhaa wa makampuni ya baadhi ya sekta ya China, na kuongeza shinikizo kwa ajira, kwa upande mwingine, wateja wa Marekani na makampuni ya uzalishaji wa sekta husika pia yatapata hasara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako