• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuondoa visa kwa watalii wanaokwenda mkoani Hainan

    (GMT+08:00) 2018-04-18 18:02:55

    China itaondoa sharti la visa kwa watalii kutoka nchi 59 wanaotaka kutembelea mkoa wa Hainan kuanzia Mei Mosi mwaka huu, ikiwa ni hatua inayolenga kuunga mkono mageuzi na sera ya kufungua mlango katika mkoa wa kusini zaidi nchini humo.

    Mamaka ya Uhamiaji ya Taifa ya China imesema, chini ya sera mpya, makundi au watalii binafsi kutoka nchi 59 zikiwemo Ujerumani, Marekani, Ufaransa, na Russia wanaweza kutembelea mkoa wa Hainan bila ya kuwa na visa na wanaweza kuishi kwa siku 30 kwa sharti la kutumia mawakala wa utalii kuandaa ziara yao.

    Kuanzia mwaka 2000, mkoa wa Hainan ulitoa visa ya siku 15 kwa makundi ya watalii kutoka nchi 21, na kuongeza nchi nyingine tano kwenye orodha hiyo mwaka 2010.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako