• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yadumisha makadirio yake kuhusu ongezeko la uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2018-04-18 18:20:11

    Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limedumisha makadirio yake kuhusu ongezeko la uchumi wa China mwaka huu na mwaka ujao kuwa ni asilimia 6.6 na 6.4.

    Shirika hilo limesema ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka 2017 kilifikia asilimia 3.8, ambacho ni cha kasi zaidi katika miaka 7 iliyopita. Ripoti ya mustakabali wa uchumi wa dunia iliyotolewa jana na Shirika hilo imekadiria kuwa, kasi ya ongezeko la uchumi la dunia katika mwaka huu na mwaka kesho kitafikia asilimia 3.9, ambayo ni sawa na makadirio yaliyotolewa mwezi Januari mwaka huu. Ripoti hiyo pia imeonya kuwa, hatua za vikwazo vya biashara na kupinga vikwazo huenda zitapunguza uaminifu na kusababisha ongezeko la uchumi wa dunia kutoka katika mchakato wa kawaida.

    Mtaalamu wa uchumi wa shirika hilo Bw. Maurice Obstfeld amesema nchi mbalimbali zinapaswa kufanya majadiliano ya pande nyingi ili kuepuka kuzidisha mgogoro kwa kutumia mfumo wa sasa wa utatuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako