• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa Elimu wa Afrika wakutana kujadili hadhi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu

    (GMT+08:00) 2018-04-18 19:22:15

    Mawaziri wa elimu kutoka nchi za Afrika watafanya mkutano wa siku tatu mjini Nairobi, Kenya wiki ijayo ili kutathmini hadhi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu kuhusu elimu katika bara hilo.

    Mkutano huo ulioandaliwa na Shirika la Elimu na Sayansi la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Umoja wa Afrika, utawakutanisha mawaziri wa elimu kutoka Afrika, watunga sera na washauri kutoka sekta ya umma na binafsi kuhusu suala la elimu. UNESCO imesema wajumbe pia watajadili, kuongeza uelewa na kubadilishana maoni kuhusu jinsi ya kuunganisha Malengo Endelevu ya Maendeleo na Mkakati wa Elimu kwa bara la Afrika katika kuboresha mifumo ya ajenda, sheria ya elimu, sera, mipango, ufadhili, usimamizi na mawasiliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako