• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Akademia ya Sayansi ya Afrika yazindua jukwaa la matokeo ya utafiti

    (GMT+08:00) 2018-04-19 08:57:39

    Akademia ya Sayansi ya Afrika AAS jana ilizindua jukwaa la kuonesha tafiti za kisasa ambazo zinakabiliana na changamoto kubwa barani Afrika kama magonjwa, njaa na mshtuko wa hali ya hewa.

    Kwa mujibu wa habari jukwaa hilo litawawezesha wanasayansi wa Afrika kuchapisha matokeo ya tafiti zao zitakazotoa taarifa zitakazoelekeza sera kwenye maeneo yanayokuza maendeleo ya uchumi wa jamii. Akademia hiyo imesema watafiti kutoka taasisi mashuhuri za kitaaluma za Afrika Kusini, Ghana na Uganda wamewasilisha makala zao kuchapishwa kwenye jukwaa hilo jipya.

    Makala zilizochapishwa kwenye jukwaa hilo zinahusu mada mbalimbali zikiwemo magonjwa ya maambukizi na mabadiliko ya hali hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako