• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yasherehekea maadhimisho ya kwanza ya uhuru bila ya utawala wa Mugabe

    (GMT+08:00) 2018-04-19 09:24:42

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana aliliongoza taifa kusherehekea maadhimisho ya 38 ya uhuru wa nchi hiyo miezi mitano baada ya kuapisha kuwa rais.

    Akihutubia kwenye uwanja wa michezo wa Harare, rais Mnangagwa amesema, hii ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kusherehekea siku hiyo bila ya utawala wa rais wa zamani Robert Mugabe, ambayo ina umuhimu wa kihistoria na kumaanisha nchi hiyo imeingia kwenye mfumo mpya wa kisiasa.

    Pia amewahimiza wazimbabwe wote wanaoishi ndani na nje washirikiane katika kujenga upya uchumi wao ulioathiriwa vibaya na vikwazo vya nchi za magharibi na usimamizi usiofaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako