• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasichana zaidi ya elfu 31 kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-04-19 09:53:30

    Wasichana zaidi ya elfu 31 watapewa chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi mkoani Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

    Mratibu wa chanjo Bibi Amos Kiteleja amesema zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 Aprili.

    Bibi Kiteleja amesema chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi itatolewa sambamba na chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa zaidi ya wiki 16.

    Wiki iliyopita, makamu wa rais wa Tanzania Bibi Samia Suluhu Hassan alizindua kampeni ya chanjo ya kitaifa inayolenga kuwapa chanjo wasichana zaidi ya laki 6 wenye umri wa miaka 14 ili kuwakinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako