• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Rayon Sport ya Rwanda, Yanga ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya zafuzu hatua ya makundi kombe la CAF

    (GMT+08:00) 2018-04-19 14:13:20

    Timu zote tatu za Afrika Mashariki zilizoshiriki mechi za jana za hatua ya mtoano ili kufuzu kuingia ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika zimefanikiwa licha ya timu zote hizo kufungwa katika mechi hizo za jana, hivyo zikasonga mbele kutokana faiada ya ushindi katika mechi za kwanza zikiwa nyumbani.

    Rayon Sport ya Rwanda imefuzu baada kuitoa Costa Do Sol ya Msumbiji licha ya kufungwa kwa magoli 2-0 ikiwa ugenini katika mechi hiyo ya jana.

    Timu nyingine iliyopenya hatua ya makundi ni Young Africans ya Tanzania ambayo jana ilifungwa goli 1-0 na Welayta Dicha ya Ethiopia ikiwa ugenini lakini kwakuwa katika mechi ya kwanza ilishinda 2-0.

    Nayo Gor Mahia ya Kenya ilifungwa kwa goli 1-0 na Supersport United ya Afrika Kusini lakini imefuzu kutokana na ushindi wa magoli 2-1 iliopata ikiwa nyumbani.

    Droo kwa ajili ya kupanga hatua ya makundi inafanyika kesho kwenye makao makuu ya CAF mjini Cairo kwa ajili ya kupanga makundi na mechi pamoja ratiba ya mechi hizo za hatua hiyo ya makundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako