• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhamishaji wa fedha kati ya China na nchi nyingine wadumisha utulivu

  (GMT+08:00) 2018-04-19 16:45:43

  Idara ya uendeshaji wa fedha za kigeni ya China leo imesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hali ya uhamishaji wa fedha kati ya China na nchi za nje imedumisha utulivu, na inakadiriwa kuwa hali hiyo itadumisha utulivu mwaka huu mzima.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, msemaji wa idara ya uendeshaji wa fedha za kigeni ya China Bi. Wang Chunying amesema, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, uchumi wa dunia umeendelea kufufuka kwa utulivu, mabadiliko ya soko la fedha duniani yameongezeka kiasi. Wakati huo huo, uchumi wa China umeendelea kuwa na mwelekeo mzuri. Takwimu zinaonesha kuwa hali ya uhamishaji wa fedha kati ya China na nchi za nje imekuwa tulivu zaidi, na uwiano wa utoaji na mahitaji ya fedha za kigeni umeimarishwa zaidi. anasema,

  "Kiwango cha ubadilishaji wa fedha za reminbi kwa dola za kimarekani kimedumisha utulivu. Idara ya uendeshaji wa fedha za kigeni inashikilia mawazo ya kutafuta maendeleo baada ya kudumisha utulivu, na kuendesha uhamishaji wa fedha kati ya China na nchi za nje kwa uwiano. Kwa jumla, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hali ya uhamishaji huo imedumisha utulivu, na kuna uwiano mzuri kati ya utoaji na mahitaji ya fedha za kigeni."

  Takwimu mpya zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu, benki za China zimenunua fedha za kigeni sawa na dola za kimarekani bilioni 434.2, ambalo ni ongezeko la asilimia 16 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na kuuza fedha za kigeni sawa na dola za kimarekani bilioni 452.5, ambalo ni ongezeko la asilimia 9.

  Bi Wang amekadiria kuwa mwaka huu, hali ya uhamishaji wa fedha kati ya China na nchi za nje itadumisha utulivu na uwiano. Anasema,

  "Ukuaji wa uchumi wa China umepata mwanzo mzuri. Katika robo ya kwanza ya mwaka huu, pato la ndani la taifa la China limeongezeka kwa asilimia 6.8. Pia tumepanga kwa makini hatua za kukinga hali hatari za kifedha, ambazo ni pamoja na kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa mambo ya fedha, na hatua hizo zimeweka msingi imara kwa ajli ya maendeleo mazuri ya soko la fedha.

  Bi Wang amesema ingawa kuna hali ya kutatanisha duniani, lakini mwelekeo mzuri wa kufufuka wa uchumi wa dunia haujabadilika. China itaendelea kufungua mlango zaidi katika soko la fedha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako