• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM yataka uratibu zaidi kutatua changamoto Somalia

    (GMT+08:00) 2018-04-20 08:44:36

    Tume ya umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imetoa mwito wa kuimarishwa kwa uratibu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini Somalia.

    Akiongea kwenye mkutano wa mafunzo kwa wadau wanaoisadia Somalia, Ofisa mwandamizi wa ofisi ya AMISOM inayoratibu mambo ya kibinadamu Bw. Abdul Diabagate, amesema kuna haja ya kuongeza shughuli za utekelezaji na ushirikiano na jamii zinazokumbwa na misukosuko mikali na majanga ya asili.

    Taarifa iliyotolewa na AMISOM baada ya mkutano huo imesema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuhimiza ushirikiano kati ya maofisa wa kiraia wa AMISOM na wadau wengine.

    Kwenye mkutano huo pia ilizinduliwa ripoti kuhusu ushirikiano wa kikazi kati ya jeshi na raia, na kuonyesha mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza taabu kwa watu walioathiriwa na ukame na waliopoteza makazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako