• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Afrika kusini mwa Sahara wakadiriwa kukua kwa asilimia 3.1 mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-04-20 09:20:18

    Benki ya Dunia imepandisha makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi wa Afrika kuwa asilimia 3.1 mwaka 2018, baada ya uchumi wa kanda hiyo kudidimia kwa miaka mitatu kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa ya kimataifa.

    Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema ongezeko la uchumi linatarajiwa kufikia asilimia 3.6 katika mwaka 2019 na asilimia 3.7 katika mwaka 2020.

    Ripoti inasema, makadirio ya ongezeko hilo yanatarajiwa kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja kutoka China na nchi zilizoendelea, na kupanua biashara ya kimataifa.

    Hata hivyo benki hiyo pia imeonya kuwa, vizuizi ya kimuundo vitazuia kasi ya ongezeko la pato la ndani la Afrika bila maendeleo mapya kupatikana kwenye mageuzi ya miundo ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako