• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yazidisha juhudi za kupambana na malaria

    (GMT+08:00) 2018-04-20 09:36:25

    Serikali ya Tanzania imesema imeimarisha hatua za kupambana na ugonjwa wa malaria, ikiwa ni pamoja na kusambaza lita 236,420 za dawa za kuua mbu kote nchini.

    Waziri wa afya wa Tanzania Bibi Ummy Mwalimu ameliambia bunge huko Dodoma kuwa dawa hizo ni kwa ajili ya kuangamiza mabuu ya mbu.

    Bibi Mwalimu amesema baada ya kuchukua hatua mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo, ikiwemo kusambaza dawa, kiwango cha malaria kimeshuka na kufikia asilimia 7.3 ya mwaka 2017 kutoka asilimia 14.8 ya mwaka 2016.

    Ameongeza kuwa mafanikio hayo yamepatikana kufuatia kuimarika kwa mifumo ya afya ya taifa, kuongezeka kwa uwekezaji katika udhibiti wa malaria, na hatua nyingine zilizochukuliwa na serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako