• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuchimba mabwawa kuboresha sekta ya kilimo

    (GMT+08:00) 2018-04-20 19:29:37

    Waziri wa Maji na Unyunyiziaji Maji Mashamba nchini Kenya Bw. Simon Chelugui amesema serikali imeweka mikakati kabambe ili kuchimba mabwawa 57 kufikia mwishoni mwa mwaka 2018 kote nchini kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo.

    Akizungumza katika kikao na bodi ya maji, Chelugui amesema mabwawa hayo yatakapokamilika yatatumika kuimarisha sekta ya kilimo ili kuangazia upungufu wa chakula nchini Kenya.Kwa sasa taifa lina asilimia 60 ya maji pekee na Bw Chelugui anasema serikali inalenga kuongeza vyanzo vya maji hadi vifike asilimia 80.

    Amesema mabwawa hayo yatatumika kuendesha miradi mbalimbali ya kilimo nchini Kenya kama vile Gulana Kulalu, na hasa inayokuza mimea kwa njia ya kuinyunyizia maji kwa mfumo wa kisasa.

    Hata hivyo, amesema watakaopokea huduma za maji sharti walipie ada kidogo ili kufanikisha usambazaji wake. Ahadi za waziri Chelugui zinajiri wakati ambapo wakazi wa kaunti za Nairobi na Kiambu wanaendelea kupitia changamoto za ukosefu wa maji.

    Baadhi ya wakazi katika kaunti hizo wanaendelea kununua maji, mtungi wa lita 20 ukiuzwa kati ya Sh20-30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako