• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Burundi, Rwanda, Tanzania na Uganda zafuzu kuingia raundi ya tatu ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U-20)

    (GMT+08:00) 2018-04-23 10:40:04

    Timu nne kutoka Afrika Mashariki, Rwanda, Burundi, Tanzania na Uganda zimefuzu kuingia raundi ya tatu ya mechi za mtoano kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika chini ya miaka 20, baada zote kujipatia ushindi wa jumla katika mechi za mtoano za raundi ya pili zilizopigwa wikendi hii.

    Timu ya taifa ya Tanzania yenyewe imefuzu kwa kuiondoa DRC kwa njia ya penati 6-5, baada ya mechi hiyo pamoja iliyopigwa mjini Kinshasa na ile iliyopigwa mjini Dar es Salaam kuisha kwa sare ya bila kufungana. Tanzania sasa itakutana na Mali katika mechi ya raundi ya tatu.

    Burundi imeondoa Ethiopia kwa magoli 3-0 kufuatia ushindi wa 2-0 ikiwa nyumbani na 1-0 ikiwa ugenini, na sasa katika raundi ya tatu itacheza na Sudan.

    Nayo Rwanda imepenya na kuingia raundi ya tatu baada ya kuiondoa Kenya kwa tofauti ya wingi wa magoli baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya bila kufungana mjini Kigali ilihali mjini Nairobi nchini Kenya zilitoka sare ya magoli 1-1, timu hiyo sasa itakutana na Zambia raundi ya tatu.

    Lakini Uganda ndiyo ilitia fora kwa kupata ushindi mnono wa magoli 8-1 dhidi ya Sudan Kusini kwa kushinda 5-1 ikiwa nyumbani na 3-0 ikiwa ugenini, sasa itakabiliana na Cameroun raundi ya tatu.

    Mechi za raundi ya tatu katikati ya mwezi mei mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako