• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mkopo wa China kwa Kenya unatarajiwa kufikia Sh trilioni 1 kupitia miradi mikubwa minne ya serikali

    (GMT+08:00) 2018-04-23 20:26:50

    Mkopo wa China kwa Kenya unatarajiwa kufikia Sh trilioni 1 ifikapo mwaka 2022.

    Hii inafuata ahadi iliyotolewa na wawekezaji wakuu Wakiuchumi kutoka Asia kuunga mkono miradi ya Jubilee ya miaka mitano ijayo ambayo inalenga kuboresha mazingira mazuri ya maisha ya Wakenya milioni 47.

    Hivi sasa, China ni mojawapo wa wafadhili wakubwa na misaada rasmi ya maendeleo nchini Kenya ambayo imefikia sh bilioni 730 ikiwa pamoja na msaada wa fedha wa sh bilioni 27.9 na mikopo ya sh bilioni 702.1.

    Fedha hizi zitatumika kwa ajenda kuu nne za serikali, ambazo Rais Uhuru Kenyatta alizindua mwezi Desemba mwaka jana.

    Lengo kuu la ajenda hzi nne ni kukqabiliana na masuala makubwa yanayo kumba wa *-Wakenya.

    Pia, inalenga kuongeza sekta ya viwanda kwa asilimia 15 ya Pato la Taifa; kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafurahia usalama wa chakula na lishe bora ifikapo mwaka 2022; afya bora kwa wote; na kujenga angalau makazi 500,000 ya gharama nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako