• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China nchini Afrika Kusini asema ushirikiano kati ya China na Afrika umefanyiwa mabadiliko na kuinuka hadi mwanzo mpya

  (GMT+08:00) 2018-04-24 16:32:34

  Balozi wa China nchini Afrika Kusini Lin Songtian amesema katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na msukumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ushirikiano kati ya China na Afrika umeboreshwa na uko kwenye mwanzo mpya.

  Balozi Lin Songtian amesema Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika lililozinduliwa katika karne ya 21 limeendeleza kwa kasi ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 10 ya mwaka 2000 hadi dola za kimarekani bilioni 17 ya mwaka 2017, huku thamani ya jumla ya uwekezaji wa China barani Afrika ikiongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 1 ya mwaka 2000 hadi dola za kimarekani zaidi ya bilioni 100. Mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China alitoa agizo la kuunganisha maendeleo ya China na maendeleo ya Afrika ili pande hizo mbili zitimize ushirikiano wa kunufaishana na maendeleo ya pamoja.

  "Pande mbili za China na Afrika zinahitajiana, kusaidiana na kupeana fursa. Ushirikiano kati ya China na Afrika umebadilika kutoka serikali kutoa misaada hadi wa kunufaishana unaofanywa na makampuni na kuamuliwa na soko. Uhusiano wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeinuka hadi kwenye mwanzo mpya."

  Mwaka 2013, rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ambalo limeitikiwa vizuri na nchi za Afrika. Pendekezo hilo limepata matunda katika baadhi ya nchi zilizofanyiwa majaribio. Balozi Lin Songtian anasema,

  "Hivi sasa, nchi tatu zinaweza kupokea zaidi ujio wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'. Moja ni Afrika Kusini, ambayo ilianza mapema kushiriki kwenye pendekezo hilo, na mafanikio makubwa yameonekana. Pili, Ethiopia ni nchi ya bara, na China imeisaidia kujenga reli ya Addis Ababa hadi Djibouti, na kusaidia maendeleo ya viwanda mbalimbali. Tatu, reli ya SGR ya Mombasa hadi Nairobi nchini Kenya haitoshi kufika Nairobi tu, bali naona inapaswa kurefushwa hadi Uganda na Rwanda. Naona huu ni ukanda mzuri wa kiviwanda kwa nchi hizo tatu, tunapaswa kuujenga na kuwa ukanda wa mfano katika ushirikiano kati ya Kusini na Kusini."

  Akizungumzia mashaka ya nchi za magharibi juu ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja", balozi Lin Songtian anaona kuwa hayo yamesababishwa na tofauti za itikadi kati ya China na nchi za magharibi. Wataalamu wa mkakati wa kijiografia wa nchi za magharibi wamegawanya nchi hiyo na kuwa sehemu kadhaa tofauti, na kuona kuna keki moja tu, nani akiikalia itakuwa kwake, lakini China inatetea kutafuta ushirikiano wa kusaidiana na maendeleo ya pamoja. Sera ya mambo ya nje ya China siku zote inaangalia maslahi ya pamoja ya binadamu. Anasema,

  "Sisi ni wageni wapywa kwa bara la Afrika. Mwaka 2000, uwekezaji wetu barani Afrika haukufikia dola za kimarekani bilioni moja. Maliasili za Afrika zimechukuliwa na nani? Ni watu wa magharibi na wakoloni wamezipora na kudhibiti kwa muda mrefu. Nigeria ni nchi yenye utajiri wa mafuta barani Afrika, pia ni nchi inayoagiza mafuta kwa wingi zaidi kutoka nje, na kwamba mafuta ghafi inayouza kwa nje hayatoshelezi nchi hiyo kununua bidhaa za mafuta kutoka nje, hiki ndicho kinyang'anyiro, lakini njia hiyo ya kikoloni bado haijakomeshwa."

  Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika mwezi Septemba mwaka huu hapa Beijing. Balozi Lin Songtian amesema huu utakuwa ni mkutano mkubwa wa kihistoria unaolenga kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya China na Afrika, na utaendelea kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika. China itatumia mkutano huo kupanga uhusiano wake na Afrika katika pande tano za siasa, uchumi, utamaduni, usalama na uratibu wa kimataifa. Anasema,

  "China na nchi za Afrika zitapanga uhusiano wao kwenye ngazi ya juu zaidi katika mkutano wa kilele wa mwaka huu. Hivi sasa kwa ujumla Afrika inaangalia upande wa mashariki, na China inapenda kuisaidia Afrika kwa udhati wa moyo kupanga vizuri mipango yao, na kusaidia nchi za Afrika kupata maendeleo ya kiviwanda, kilimo na upanunzi wa miji, na kuzisaidia kupata maendeleo endelevu kwa kujitegemea. Nina matumaini makubwa na mkutano wa kilele wa mwaka huu, na inaaminiwa kuwa mafanikio na uzoefu wetu wa miaka 40 ya mageuzi na ufunguaji mlango utajenga mustakabali mzuri kwa watu wa China na Afrika."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako